Mauaji ya Wambui: Polisi kumuachilia huru Joseph Kori

Joseph Kori ambaye ni mume wa mwendazake Mary Kamangara, Alhamisi ilikuwa siku ya kueka katika kumbukumbu zake za maisha hii ni baada ya kutolala korokoroni kwa maana aliweza kuachiliwa huru.

Alihusika na mauaji ya mke wake wiki tatu zilizopita huku mpenzi wake akiwa ni yeye aliyemuua Mary Kamangara mke wa Kori.

Mpenzi wake Kori Judy Wambui bado yumo mikononi mwa polisi katika kituo cha polisi cha Muthaiga. Familia ya Wambui iliweza kusema kuwa walikuwa wanangoja Kori aachiliwe ili waweze kumzika Wambui.

"Katika uchunguzi ambao ulifanyika na kuonekana kuwa Kori hakuweza kuhusika katika mauaji ya mke wake, sisi kama familia tuliamua kumngoja aweze kuachiliwa huru ili aweze kumzika mke wake, nyumbani kwake Mweiga kaunti ya Nyeri," Bi Esther Kamangara alisema.

Februari, 13, Mahakama ya Kiambu iliweza kuambia sekta ya DCI iweze kuwaeke wawili hao korokoroni, pamoja na dereva ambaye alikuwa amembeba mwendazake Mary, kwa siku 14 ili wachunguzi waweze kuendeleza na uchunguzi wao.

Awali Joseph Kori aliweza kuambia mahakama imuachilie kwa dhamana kwa maana uchunguzi haukuweza kuonyesha kuwa alihusika katika mauaji ya mke wake.

Mkuu wa DCI George Kinoti aliweza kuambia Inspekta John Wahome aweze kuongoza uchunguzi wa mauaji hayo, wakati wa mauaji hayo uchunguzi ulionyesha kuwa Kori alikuwa katika kaunti ya Kajiado maeneo ya Ngong.

Aliweza kutoka maeneo hayo saa tatu usiku.