Mawasiliano ya simu ya mwisho ya Uhuru na Bob Collymore (Yaliyomo)

The-late-Bob-Collymore-1068x601
The-late-Bob-Collymore-1068x601
Rais Uhuru Kenyatta ameweza kueleza mwanzo mwisho kuhusu simu yake ya mwisho na marehemu Bob. Kiongozi wa taifa alikuwa akimuomboleza kiongozi huyu wa kampuni kubwa zaidi afrika mashariki ya Safaricom.

“Wiki 3 tatu nyuma nilikuwa katika ziara nchini Canada...Bob alinipigia simu saa nane asubuhi. Siku ya pili nikachukua simu yake na nikamuuliza, "Bob, mbona unanipigia simu saa nane?" Alieleza Uhuru.

Soma hapa :

Collymore akamjibu , ‘Ahhh, Sikujua umesafiri.’  Rais alimueleza kuwa amesafiri ila akirudi nchini atampigia.

"Ila akazidi kuniambia, nina kitu cha dharura ningependa kusema nawe japo naweza nikasubiri mpaka urejee nchini. Ningependa nikuambie kuwa niliapa kwako kwamba nitaiongoza kampuni hii kwa mwaka mmoja zaidi ila nafikiri nitavunja kiapo hicho." alieleza Uhuru.

"Nikamuuliza mbona?" Akasema kuwa tutazungumza nikirejea.

"Nikawa najiuliza maswali mengi. Collymore akaongeza kusema kuwa " Tafadhali usiambie yeyote nilichokisema. Tutazungumza ukifika."" alisimulia Uhuru.

Aliporejea nchini Rais alifika kwake Bob.

"Nikafika kwake nikampata ametulia na akaniambia kuwa atavunja kiapo chake kwangu huku akionyesha tabasamu. Nikafikiria labda Wambui huenda amemuweka presha..." alifunguka Rais.

“Sivyo unavyowaza. Ila nadhani sina wiki mbili za kuishi. Nimekata tamaa. Nimejaribu kila kitu ila wakati wangu umefika." Bob Collymore.

Soma hii:

“Kwa hivyo tukatulia pale kwake tukizungumza ila swali langu kuu lilikuwa mbona alikuwa anaijali sana Safaricom ila sio yeye." Uhuru.

Ila Bob akamjibu "Maisha yangu yamefika mwisho na nimekubali. Ninachotaka kujua ni maisha ya usoni ya Safaricom yatakuwaje."