Mawazo na Kukosa pesa: Dakika za mwisho mwisho kabla Papa Dennis kujirusha

Papa Dennis na kakake Simon
Papa Dennis na kakake Simon
Msanii wa Gospel  Papa Dennis huenda alikuwa na mawazo kupindukia na matatizo ya kukosa pesa  ,jamaa yake ,rafiki na msimamizi nyumba  alikokuwa wamesema .

Majirani na  msimamizi wa nyumba alioishi Dennis wamesema nyoashukuru’  aliyepatikana amefariki  siku ya jumamosi  alikuwa    matatizo ya hela na huenda  yalichania hatua yake kujiua .

“ Mwenye nyumba ALIKOISHI MTAANI JAMHURI ALIKUWA AMEMFUNGIA NYUMBA  NA WATU ALIOKUWA AKIISHI NAO KWA MUDA WALIKUWA WAKIMPIGA . HAPO NDIPO  MMILIKI WA STUDIO ILIYOKO JENGO LA KIRIMA ALIMTAKA AJE AISHI HUKO KWA MUDA AKITULIZA FIKRA ZAKE'  Jamaa yake wa karibu amesema

 Papa Dennis  pia inaripotiwa alikuwa na matatizo na mpenzi wake wa miaka miwili ambaye ni muigizaji  katika kipindi kimoja  cha televisheni humu nchini .

“ Siku ya ijumaa mwendo wa saa tano asubuhi papa dennis alimpigiasimu mjukuu na kumwambia kwamba kuna waliokuwa wakipigana katika nyumba iliyo na studio’ msimamizi wa nyumba hiyo amesema .

 “ Mmiliki wa studio alinipia simu  na nilipobishamlango ,Dennis ndiye alaiyefungua’

Msimamizi huyo wa nyumba amesema baadaye Dennis alichukua simu yake na kupanda pikipiki akielekea upande wa Muthaiga katika barabara ya Thika .Papa Dennis  alirejea baadaye  na kakake pacha  Simon Mwangi akajiunga naye  na producer ili waendelee kurekodi katika studio hiyo .

“ Kisha aliichukua simu yake na chaja  katikati ya kurekodi na kutoka akisema kakake na producer walikuwa wakimpa wakati mgumu’. Msimamizi huyo wa nyumba baadaye siku ya ijumaa aliarifiwa na baadhi ya wapangaji kwamba kuna mtu  aliyeruka kutoka upande wa pili wa jingo  kutoka ghorofa ya nne .“ Nilimuambia kakake na  maneja wa studio na mmiliki wa studio kwamba mmoja wa rafiki  yao ameruka kutoka ghorofa ya nne’ msimamizi huyo amesema .

 “ Hatuna uhakika wa jinsi alivyofika upande wa pili wa mwisho wa kabisa wa jingo hilo kwa sababu milango yote ya kwenda upande huo ilikuwa imefungwa . chaguo jingine na kupitia nyumba ya mtu au kupitia paa ,jambo ambalo ni gumu’ msimamizi huyo amesema .