Mayooo! Tazama picha za Kasisi Richard Onyango Oduor aliyepatikana na virusi vya Corona Siaya

onyango
onyango
NA NICKSON TOSI

Picha za Kasisi Richard Onyango Oduor aliyepatikana na virusi vya Corona zimeibuka mitandaoni masaa machache tu baada ya Kasisi huyo kuwekwa chini ya uangalizi .

Kasisi Onyango mwenye makao Rome Italia ,aliwasili nchini mnamo Machi 11 mwaka huu na kuongoza misa katika kanisa la katoliki la Holy Family Nairobi eneo la Utawala.

Baada ya kuongoza misa hiyo,Onyango alisafiri hadi Ugunja ,Siaya,akitumia basi la shirika moja nchini ambapo alikuwa anaenda kuongoza hafla ya mazishi tarehe 14 Machi.

Kasisi Richard Oduor alipatikana na virusi vya Corona Machi 22 na sasa serikali imeanzisha hatrakati za kuwatafuta watu ambao alikaribiana nao alipokuwa Siaya na eneo la Utawala.

 
Zifuatazo ni baadhi ya nyingine ambazo zinaonyesha Kasisi Richard Oduor akijumuika na baadhi ya watu katika eneo la Ugunja ,kaunti ya Siaya.
Serikali ilikuwa imetoa ilani kwa kila msafiri anayetua nchini kuwekwa chini ya karantini kama njia ya kutathmini wale walioambukizwa virusi vya Corona.
Kufikia sasa ,taifa la Kenya limesajili watu 16 ambao wamepatikana kuwa na virusi hivyo vya Corona.