Mbio za nyani huishia Jangwani mke wa Ali Gichunge akamatwa

violet kemunto
violet kemunto
Mke wa gaidi aliyeuliwa katika shambulizi la  DusitD2 Ali Gichunge akamatwa katika kaunti ya Makueni  ijumaa asubuhi.

Kemunto  Violet Omwoyo anatarajiwa kupelekwa mbele ya korti.

Swali kuu ni je Kemunto alikuwa mafichoni wapi baada ya kukamatwa na polisi,alikamatwa baada ya siku zilizozidi tano.

Violet aliishi na mumewe Ali Salim Gichunge ambaye polisi wanaamini kuwa yeye ndiye alikuwa mkubwa katika shambulizi hilo.

Waliishi katika mtaa wa Guango tangu mwaka jana marchi 21 ambapo walinzi walisema kuwa Gichunge alikuwa anapenda kuwasalimia mara alipokuwa akipita.

Kemunto alinasya kupitia mtandao wa kijamii wa[facebook] almaarufu Pseudo alipokuwa anauza nyumba akisema kuwa wenyewe wanahama Nairobi.

Washukiwa wengi wako mikononi mwa polisi na kupelekwa mbele ya korti kwa mashtaka au madai kuwa walihusika katika shambulizi hilo.

Ijumaa iliyopita korti ilisema wako na washukiwa ,5,na watakaa korokoroni kwa siku,30, ili kuwezesha polisi kumaliza uchunguzi wao.

washukiwa hao nikama wafuatavyo;Joel Nganga,Oliver Muthee,Gladys Kaari,Guleid Abdikahim na Osman Ibrahim.

Pia DPP anampango wa kuwatoza benki ya DTB kwa  kuwasaidia na kwa kuruhusu shambulizi,mshukiwa aliweza kutoa shillingi millioni 9 kwa siku moja.

Hassan Nur aliweza pia kutoa shillingi laki 4 mara tatu kwa muda mfupi januari na kisha kuongezea kutoa shillingi laki 100,000 siku hiyo hiyo.

Kweli akiyesema kuwa mkono wa polisi ni mrefu au siku za mwizi na arobaini hakukosa bali alisema ukweli mtupu.

Kitengo cha kuoambana ugaidi kilisema kuwa pesa hizo zilitumwa kutoka Afrika kusini na kisha kutolewa Somalia,DPP Alhamisi alisema kuwa korti inatayarisha mashtaka dhidi ya benki ya DPP na wakubwa wake.