Mbona niombe msamaha kwa kumualika Akothee bungeni? - Sankok

sankok (1)
sankok (1)
Mbunge David Sankok amekiri kuwa hawezi omba msamaha kwa kumualika Kidosho bi Akothee, mwanadada mwenye miguu mirefu bungeni ili aweze kupatana na wabunge wenzake na kuomba ushirikiano wao katika mradi wa kusaidia wana Turkana.

Haya yanajiri pindi tu baada ya msanii huyo kuzua rabsha bungeni, Jumanne mchana kwa kuingia akiwa amevalia sketi fupi.

Hapo ndipo walinda lango pamoja na wengi waliokuwa bungeni wakabaki wameduwaa na kumzuia asiingie hoteli iliyo bungeni.

Sankok alisema kuwa alipoenda kumchukua Akothee katika lango kuu la bunge alimuangalia na kudhibitisha kuwa alikuwa amevaa vyema. Licha ya hilo, anasema alipofika bungeni hapo ndipo aliambiwa kuwa sketi yake lazima iwe chini ya magoti.

Sankok alieleza,

Mbona niombee msamaha kwa kumleta mkenya mrembo mwenye miguu mirefu ili awaalike wabunge wenzangu waweze kumuunga mkono na kuchangia mipango yake ya kusaidia wanaoumia, Turkana.

Akothee alikuwa amevalia vyema zaidi kwani alikuwa amevalia mavazi rasmi.

Nilipoenda kumchukua katika lango kuu nilimchambua kutoka pembe zote na alikuwa amevalia vyema, lakini nilipofika hapa wakasema kuwa sketi yake lazima iwe chini ya magoti.

Baada ya vurugu kidogo na wanasheria wa bungeni, Akothee alikubaliwa apite na kuingia bungeni bila walinzi wake.
Zaidi ya hayo, wanasheria wa bungeni walijaribu kumpa kikoi ajifunge lakini mipango yao ikaambulia patupu. Akothee alikuwa amevalia mini sketi ya rangi ya kijani ambayo haikuwa karibu hata kufika magotini.
Baada ya dakika chache za kubishana na wanasheria wa bungeni, Akothe alipewa ruhusa na kuambiwa atumie mlango wa nyuma kuingia kwenye hoteli hiyo ya bungeni.