Mbona serikali hupuuza uwezo wa sekta ya Jua kali nchini?+Podi ya kuchanganua tatizo hilo

icu beds
icu beds
Wiki  hii kumekuwa na mhemko sana mtandaoni baada ya serikali kuagiza kwamba itanunua vitanda 500 vya ICU kutoka kwa vijana wawili Mungai Gathogo, 26,  na  Joseph Muhinja, 35,  ambao wana makao yao huko Githunguri kaunti ya Kiambu.

Hatua hiyo ilizua lalama sana kwani wa kwanza aliyeibuka na   biashara ya kuunda vitanda vya ICU  Meshack Otieno aliachwa kavu kavu. Wengi walihisi kwamba serikali ingegawanya tenda hiyo kati ya makundi ya vijana ili pawe na usawa.

&t=40s

Katika Podi hii tunajadili mbona kwa muda mrefu serikali na wakenya kwa jumla wamekuwa wakipuuza vitu vinavyotenegezwa humu nchini na badala yake kuamini sana vitu vinavyoagizwa kutoka nje. Je,vitu vya nje ni bora zaidi kuliko vyetu au kuna kasumba ya kutojiamini?

Kuanzia tenda za ujenzi wa miradi mikubwa, kandarasi za kuagiza mashine za gharama ya juu zinazoweza kuundwa humu nchini hadi kuagiza nguo kutoka nje, Kenya imekuwa nchi ya kuagizaagiza ilhali uwezo tunao wa kutenegeza kila tunachokihitaji.