Mbona tusitii masharti! Mwanamke aliyesafiri kutoka Nyali hadi Kisii apatikana na corona

FILE PHOTO: Test tube with Corona virus name label is seen in this illustration taken on January 29, 2020. REUTERS/Dado Ruvic/File Photo
FILE PHOTO: Test tube with Corona virus name label is seen in this illustration taken on January 29, 2020. REUTERS/Dado Ruvic/File Photo
Maafisa wa afya kaunti ya Kisii wamesema mwanamke wa miaka 34 kutoka eneo la Nyachogochogo, Nyamache  amepatikana  na virusi vya corona.Mgonjwa huyo ambaye alipatikana na virusi hivyo alikuwa amesafiri kutoka Nyali kaunti ya Mombasa na alikuwa amewekwa chini ya Karantini kwenye kituo cha KMTC kaunti hiyo.

Maafisa hao aidha wamesema watu wengine 36 waliokuwa wametangamana na mwathiriwa wameopatikana na kuwekwa chini ya karantini.

Gavana wa kaunti hiyo James Ongwae ameliambia jarida la The Star kuwa jamaa mwengine aliyekuwa amesifiri kutoka eneo la Namanga alipatikana na virusi hivyo baada ya maafisa wa afya kumtafuta kabla ya kutangamana na watu wengine.

Katika kisa cha hivi sasa ,mwanamke huyo sasa anasemekana aliingia Kissi Mei 19n mwezi huu na kuelekea moja kwa moja hadi nyumbani kwake Nyachogochogo eneo la Nyamache .

Ongwae sasa amesema wamechukuwa hatua kama kaunti ili kufunga mipaka yote inayotumiwa na watu wanaotoka katika kaunti zilizoathirika zaidi na virusi hivyo.

" It is definitely worrying us because both cases are people who broke curfew and lockdown guidelines," "As a county we urge that there be strict checks to ensure only those offering essential services are allowed to cross the red lines."amesema Ongwae.