Wakenya Wengi wanajiuliza maswali kuhusu hatua ya Uganda kwenda Tanzania katika mradi wa ujenzi wa kilomita Zaidi ya 1400 za bomba la mafuta na kuiacha Kenya ambayo ilitarajiwa kuhusishwa na mradi huo . Sikiliza podcast nzima kuhusu mradi huo na jinsi wakenya walivyokerwa kwa kuachwa nje.
&t=15s
Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni wiki jana walisaini mkataba wa mradi huo wenye gharama ya dola bilioni 3.5 ambao utaiwezesha Tanzania kuunda nafasi elfu 18 za kazi kwa raia wake .Je, ndio sababu ya masaibu hayo? Uganda imesema bomba hilo lingegharimu kiasu cha juu cha pesa upande wa Kenya na pia rais Museveni alikuwa na hou kuhusu hali ya usalama nchini Kenya .