Wanaume wa Lamu wahimizwa kuendelea kuzaa na wake zao

karaya
karaya
Jane Karaya ambaye ni afisa katika hazina ya usawazishaji wa maendeleo nchini - NGAAF, anahimiza wanaume katika kaunti  ya Lamu kuzidi kuzaa na wake zao.

Akiongea mjini Lamu, Karaya alisema kuongeza idadi ya watu katika kaunti hiyo ya Lamu kutachangia serikali kuongeza pesa zinazotengewa  shirika hilo (NGAAF).

 "Hatutaki wanaume kulala usiku, mzae watoto. Tunahitaji idadi ya watu kuongezeka kama hiyo ndio njia pekee ya kuongezewa pesa zaidi," Karaya alisema.

Kaunti ya Lamu kwa muda mrefu limekuwa ikipata pesa kidogo chini ya hazina ya NGAAF kutokana na idadi ya watu.

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti hiyo Ruweida Obbo amekuwa akipigania kuongezwa kwa fedha za NGAAF katika kaunti hiyo hadi shilingi milioni 14 kwa kila jimbo kutoka shilingi milioni 7 kiasi kinachotolewa kwa sasa.

Obbo anasema lengo kuu ni kuboresha maisha ya wanawake, vijana, na wale wote walio na mahitaji mengine katika eneo hilo.

 Mhariri: Davis Ojiambo