badi 2

Mbunge Alice Wahome aishtaki Serikali kuhusu kuruhusiwa kwa Mohammed Badi katika baraza la mawaziri

Mbunge wa Kandara Alice Wahome ameishtaki serikali kuhusu kujumuishwa kwa mkurugenzi wa maamlaka ya NMS Mohammed Badi katika baraza la mawaziri .

badi

Gavana Korane aachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3.25 azuiwa kwenda afisini mwake

Katika kesi yake mbunge huyo  amesema mwaliko aliopewa Badi unakiuka katiba  na hivyo basi anataka agizo kutolewa kumzuia mkuu huyo wa NMS  dhidi ya kuhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri .

Kulingana naye ,serikali ilikiuka katiba kwa kumruhusu mwanajeshi huyo kuhudhuria mikutamo ya baraza la mawazi .Badi maajuzi amekubaliwa kwenda katika mikutano yote ya mawaziri  baada ya kula kiapo cha kuweka siri katika Ikulu ya Nairobi .

Mkuu huyo wa NMS ana jukumu la kuliboresha jiji la Nairobi baada ya serikali ya kaunti ya Nairobi kuikabidhi serikali kuu baadhi ya majukumu yake katika makubaliano kati ya gavana Mike Sonko na Rais Uhuru Kenuyatta .

Je, Kuna tatizo mwanamke akimzidi mume umri?+Podi ya Yusuf Juma

NMS  Iliwekwa afisini machi tarehe 18 mwaka huu  na kuanza kutekeleza majukumu manne muhimu ya  Afya ,huduma za usafiri ,ujenzi  na mipango na maendeleo kutoka kwa serikali ya kaunti .

 

 

 

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments