Mbunge Ndindi Nyoro avunja kimya chake kuhusiana na ugavi wa mapato wa kaunti

a2c401ef380b65ed(1)
a2c401ef380b65ed(1)
Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amevunja kimya chake kuhusiana na mfumo wa ugavi wa mapato uliokubaliwa na seneti mnamo Alhamisi, Septemba 17.

Mbunge huyo wa Tangatanga alilalamika vikali akisema maeneo ya Mlima Kenya yamefinywa na kwamba hamna cha kusherehekea.

Kupita kwenye mitandao yake ya kijamii Nyoro alizungumza kuhusiana na mjadala wa ugavi wa mapato ambao ulizua mgawanyiko mkubwa bungeni, Nyoro alisema deep state na Ikulu zimeacha Mlima Kenya katika hali mbaya zaidi ya ilivyokuwa awali.

"Kaunti zetu 11 ambazo ni Tharaka Nithi, Nyeri, Embu, Murang'a, Kiriyaga, Laikipia, Nyandarua, Meru, Kiambu, Nakuru zenye idadi ya watu milioni 10.78 walipata KSh 74.9 bilioni kumaanisha kila mkazi alipata KSh 6,800." Alisema Ndindi.

Mfumo uliopendekezwa ulizingatia vigezo nane vya ugavi wa rasilimali ambapo idadi ya watu ilitengewa kiwango cha juu zaidi cha asilimia 18.

Afya ilipewa 17%, kilimo 10%, maendeleo ya mijini 5%, barabara 8%, kiwango cha umaskini 14%, misingi 20% na ardhi kwa 8%.