Mbunge Ndindi Nyoro kufikishwa mahakamani hii leo

nyoro
nyoro
Mbunge wa Kiharu MP Ndindi Nyoro anatarajiwa kortini hii leo baada ya kukamatwa jana usiku katika kukuru kakara iliyoshuhudiwa jijini Murang'a.

Kukamatwa kwake kulikamilisha mchezo wa paka na panya dhidi yake na maafisa wa polisi uliochukua masaa 24, baada ya mzozo ulioshuhudiwa katika kanisa moja siku ya Jumapili.

Viongozi wanaoegemea upande wa naibu wa rais William Ruto walikongamana katika kituo cha polisi cha Kamukunji, Nairobi ambapo wanaamini mbunge Ndindi atasafirishwa kutoka Murang'a.

Walidai Ndidi awaachiliwe uhuru huku wakiwalaumu afisa wa polisi kwa kuwatisha wanasiasa wanaoegema upande wa Ruto.

Aliwachiliwa usiku wa manane na kuamrishia ajifikishe kortini. Alikuwa amekamatwa akiwa katika mkutuno mjini Murang'a, mkutano uliopeperushwa moja kwa moja runingani.

Nyoro  alikuwa amezozana na mbunge mteuliwa Maina Kamanda Jumapili huku akimlaumu kwa kuongoza shughli za Harambee katika ngome yake bila kumpa mualiko.

Kisa hicho kilifanyika katika kanisa la kikatoliki la Gitui wakti Kamanda wa kundi la Kieleweke alikuwa anaongoza shughli za kuchangisha fedha.

-Cyrus Ombati