Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi atafikishwa katika mahakama ya Nakuru leo baada ya kujisalimisha kwa polisi siku ya jumamosi huko Eldoret .
Sudi anatarajiwa kujibu mashtaka ya uchochezi kuhusu matamshi yake ambayo yamelaaniwa na viongozi mbali mbali na alikuwa akisakwa na polisi kabla ya kujisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi cha Langas Eldoret .
Alikamatwa na polisi ambao baadaye walimsafirisha kwa helikopta hadi Nakuru .kundi la mawakili wake likiongozwa na Gladys Shollei linasisitiza kwamba mbunge huyo hakutamka neno lolote la uchochezi na wako tayari kumtetea mahakamani .
Sudi anashtumiwa kwa kutoa matamshi makali dhidi ya rais Kenyatta na mamake rais , mama Ngina Kenyatta .