MP

Mbunge Oscar Sudi kusalia korokoroni kwa siku zingine7

Mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi atasalia korokoroni kwa siku nzingine saba, huku akingonja uamuzi wa kutoka kwake kwa dhamana, Sudi alishtakiwa kwa tuhuma za uchochezi.

Maagizo hayo mapya yametolewa na mahakama ya Nakuru ili wapelelezi waweze kukamilisha uchunguzi wao.

Kikosi:Tazama picha za Viongozi waliofurika mahakamani kumpiga jeki Oscar Sudi

Jumatatu wiki hii mahakama hiyo ilitoa agizo mbunge huyo kusalia mikononi mwa polisi kwa siku mbili ili aweze kungoja uamuzi wa korti kuhusu kuachiliwa kwake kwa dhamana.

Sudi alipelekwa katika kituo cha polisi cha Nakuru ambapo alitoroka kukamatwa kwake wikendi iliyopita kisha baaaye akajilazimisha mikononi mwa polisi.

Mbunge Oscar Sudi kufikishwa kortini leo

Mashtaka yalikuwa yameuliza kusalia kwa Sudi kwa siku 14 ili uchunguzi ukamilike bali wakili wake aliwasilisha ombi la kuachiliwa kwake kwa dhamana

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments