Mbunge Sudi kusalia korokoroni kwa siku 7 zaidi

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi  atasalia korokoroni kwa siku saba Zaidi.

Sudi  alikuwa tayari amelala seli kwa siku mbili Zaidi katika kituo cha polisi cha Central mjini Nakuru akingoja kutolewa kwa uamuzi wa iwapo angeachiliwa kwa dhamana .

Sudi  alifikishwa mbele ya  hakimu mkuu wa nakuru  Josephat Kalo  kwa kikao  cha ombi la upande wa mashtaka unaotaka kumzuilia kwa siku 14 ili kuruhusu uchunguzi kufanyika .

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Daniel Karuri unataka muda Zaidi ili kukamilisha uchunguzi wake dhidi ya makosa yanayodaiwa kutekelezwa na mbunge huyo .

Karuri amepinga kuachiliwa kwa mbunge huyo kwa dhamana akisema  anachunguzwa kwa matamshi ya chuki  ,kumshambulia afisa wa polisi na kumiliki bunduki bila leseni  kando na kukataa kukamatwa .