Mbunge wa Sirisia John Walukhe ahukumiwa miaka 7 gerezani kwa kosa la ufisadi

Waluke
Waluke
Mbunge wa Sirisia John Walukhe na mfanyibiashara Grace Wakhungu wamehukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani au faini ya zaidi ya shilingi milioni 727.7 kwa kosa la kulaghai serikali pesa.

Walukhe na Wakhungu walipatikana na hatia ya kulaghai serikali takriban shilingi milioni 300 kuhusiana na sakata ya mahindi.

Hakimu wa mahakama ya kukabiliana na ufisadi  Elizabeth Juma siku ya Jumatatu alimpata na hatia Walukhe na mshtakiwa mwenzake Grace Wakhungu kwa kupokea takriban shilingi milioni 300 kutoka bodi ya kitaifa ya nafaka ya mazao NCPB mwaka 2004.

Wakhungu ameorodheshwa kama mkurugenzi wa kampuni ya Erad General Suppliers.

Katika uamuzi wake hakimu Juma alisema kwamba kulikuwepo na ushahidi wa kutosha kuonysha kwamba wawili hao walitumia stakabadhi ghushi kupokea malipo ya ada kuifadhi mahindi kutoka Ethiopia.