Mkusanyiko wa Habari zaidi
Itakuwa afueni wa wadhamini wa mikopo endapo mswada unaolenga kuwalinda utapitishwa kuwa sheria .mswada huo uliopendekezwa na mbunge wa juja Francis waititu unapendekeza kwamba aliyetia sahihi kudamini mkopo wa mtu hafai kupokonywa mali yake kwa haraka endapo njia zote hazijatumiwa kumfanya aliyekopa pesa kuzilipa kwanza .
Serikali imejitenga na matamshi ya mbunge wa starehe Charles kanyi kwa jina la usanii jaguar kwamba wafanyibiashara wa kigeni walioko jijini wanafaa kurejeshwa makawao . jaguar alinaswa katika video akitoa vitsho vya kuwaongoza wafanyibiashara wa hapa Nairobi kuwaondoa wenzao kutoka nje za kigeni .tayari bnge la taifa jirani la Tanzania limelalamikia vikali matamshi hayo .
Wanaharakati wa kupambana na saratani chini ya vugu vugu la Network of Cancer organizations wamesema madai ya madai ya madakari wa kanis aa katoliki kwamba chanjo cha HPV itaongezwa visa vya ugonjwa huo yanapotosha . mwenyekiti David Makumi amesema uchunguzi wa kina umeonyesha kwamba chanjo hiyo huzuia ukuaji wa chembe za virusi hivyo HPV na hivyo basi njia bora kuzuia ugonjwa huo .
Wakenya katika maeneo ya mashinani wataweza kupata matokeo ya vipimo vya kiwango cha virusi vya HIV katika muda wa dakika 70 baada ya kuidhinishwa kwa vifaa rahisi vya kubebwa vya kupima vilivyotolewa na shirika la WHO . Hapo awali sampuli zilichukuliwa na kupelekwa kwa shirika la kemri na matokeo kutolewa baada ya wiki mbili . vifaa hivo vya WHO kwa jina M-PIMA vitawasaidia wakaazi wa maeneo ya mbali huko mashinani .
Peter Mbithi atafahamu hatma yake leo baada ya kuonyesha nia ya kutaka kuendelea kuhudumu kama mhadhiri mkuu wa chuo kikuu cha Nairobi .Baraza la chuo hicho linaloongozwa na Julia Ojiambo litafanya uamuzi wake leo .hatamu ya Mbithi inafika tamati januari mwakani .
Mshukiwa mmoja wa ujambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika eneo la jomvu huko Mombasa . Polisi walifahamishwa na wakaazi kwamba mshukiwa huyo alikuwa akilimiki bunduki kinyume cha sheria na wakaanza kumchunguza . Alianza kuwafyatulia risasi polisi walipompata nyumbani kwake .
Kenya leo inajiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya na ulanguzi wa mihadarati .kauli mbiu ya maadhimisho ya siku hii mwaka huu ni ‘afya kwa haki na haki kwa afya’. Umoja wa mataifa umesema kauli mbiu hiyo inawiana na maazimio ya kukabiliana na mihadarati kwa njia ya jumla kuhusisha afya ,haki na taasisi ya huduma za kijamii .