Mbunge wa Starehe 'Jaguar' kuchunguzwa kwa matamshi

'Jaguar' achunguzwa kwa matamshi shidi ya wawekezaji.

Mbunge wa Starehe Charles Kanyi anachunguzwa baada ya kutoa matamshi yaliyoonekana uwatishia wawekezaji wa kigeni jijini Nairobi. Msemaji wa serikali Cyrus Oguna ameyakashifu matayamshi ya mbunge huyo na kuwahakikishia usalama wawekezaji hao. Kanda ya video inayomwonyesha Jaguar akitishia kuwafurusha raia hao imesambaa mitandaoni.

Vijisanduku vya hewa katika gari la marehemu Gakuru havikufanya kazi.

Vijisanduku vya hewa ndani ya gari la aliyekua gavana wa Nyeri Wahome Gakuru havikufanya kazi ipasavyo, wakati ajali iliyopelekea kifo chake ilipotokea, shahidi mmoja alifichua jana. Shahidi huyo wa kwanza katika uchunguzi kuhusu kifo cha gavana huyo alisema, vijisanduku hivyo upande wa dereva vilifabya kazi punde tu baada ya ajali hio kutokea, na kumpelekea dereva kunusurika bila majeraha.

Ada ya kuegesha magari jijini Nairobi kupanda kuanzia mwezi ujao.

Wenye magari ambao huegesha katikati mwa jiji watagharamika zaidi kwani ada za kila siku za kuegesha magari zitapanda kutoka shilingi 200 kuanzia mwezi ujao. Katika bajeti ya kaunti ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 gavana Sonko ananuia kukusanya shilingi bilioni 17.3.

Chanjo ya maradhi ya Meningitis yazinduliwa Lodwar.

Chanjo ya maradhi ya meningitis imezinduliwa katika hospitali ya rufaa ya Lodwar kuwalenga watoto wa umri wa mwaka mmoja na zaidi. Chanjo hio pia itapewa watu wazima walio chini ya umri wa miaka 30, kwani wako katika hatari zaidi ya kufariki kutokana na mkurupuko wa maradhi hayo.