Mbwa msaliti: Wezi wamlisha mbwa githeri kabla ya kufanya uhalifu

Msanii aliyeimba na kusema kuwa katu hatohama Kenya alikuwa na sababu zake, na kwa upande wangu, sababu zangu huongezeka kila uchao.

Hii ni baada ya kisa kimoja kuripotiwa cha mbwa ambaye alilishwa sahani ya githeri na wezi kabla yao kuponyoka na bidhaa zenye dhamani isiyojulikana.

Kulingana na jamaa kwa jina Mac Otani, kisa hiki kilitokea katika kaunti ya Nyandarua wikendi iliyopita huku wengi wakimlaumu mbwa huyo kwa kumsaliti mwenyewe kwa ajili ya sahani ya githeri.

Otani alichapisha habari hii kwa mtandao wake wa Twitter akisema,

Thugs break into a home at Muteng'uri in Nyandarua County and feed dog githeri before making away with items of unknown value.
Kisa hiki kiliwaacha wenyeji wa kijiji cha Muteng'uri na mshangao mkuu kwani inasemekana kuwa mbwa huyo alikuwa ameshiba kupindukia na hangeweza kuwika. Hilo lilitendeka huku wezi hao wakivunja nyumba kadha wa kadha bila haraka.

Familia hiyo sasa imebaki isijue cha kufanya kwani sasa wamesalia wakihesabu hasara huku wasielewe jinsi wezi hao walivyoweza kumbabaisha mbwa na sahani ya Githeri.

Tazama picha zifuatazo zinazo onesha uhalifu uliotekelezwa na wezi hao.