Mwakilishi mteule Mary Ogodo alivunjika mkono wake wa kushoto baada ya kizaazaa kuzuka katika bunge hilo kwa sababu ya mgawanyiko kuibuka kuhusu hoja ya kutaka kumuondoa madarakani gavana Obado .
Patashika hiyo ilimfanya Sajini mkuu kukimbia na kifaa cha maamlaka ya bunge m na kuwacaha waakilishi wengine wakipambana na wenzao katika bunge la kaunti huku chupa za maji zikirushwa na viti vikitumiwa kama silaha .
Ogodo alikimbizwa katika hospitali ya kimishenari ya St Joseph ambako anapokea matibabu .
Malumbano yalianza wakati wa kikao cha asubuhi wakati mwakilishi wa wadi ya North Kanyamkago George Omamba alipopata agizo kutoka kwa mahakama kuu ya Mgori kumrejesha kama naibu wa spika .
Omamba alikuwa amefurushwa na wenzake kupitia kura mwaka jana pamoja na karani wa bunge Tom Opere huku mwakilishi wa wadi ya Bukira mashariki Mathews Chacha na Emmanuel Abala wachukua hatamu kwa muda
Malumbano yalizuka wakati waakilishi watano wanaomuunga mkono Obado wakiongozwa na mwakilishi wa Kaler Thomas Akungo walipoingia bungeni na kujaribu kukatiza kikao kilichokuwa kikiendelea .