Bethwel Mwambu

MCA fulani avamiwa huko Bungoma

Mwakilishi wa wadi ya Mbakalo katika bunge la kaunti ya Bungoma Bethwel Mwambu ametaka usalama kuimarishwa haswa kwa viongozi baada ya gari lake kugongwa mbele na silaha isiyojulikana na mtu asiyejulikana hapo jana usiku kwenye barabara kuu ya kutoka Bungoma kuelekea Webuye.

Akiongea na wanahabari baada ya kuandikisha taarifa kwenye kituo cha Webuye hii leo, Mwambu anahoji kuwa hamlaumu mtu yeyeote japo akataka maafisa wa polisi kuhakikisha usalama unaimarishwa katika kaunti ya Bungoma.

Mwambu anasema kuwa hafahamu kama ilikua kisa cha kawaida ama ni yeye ndiye alikua analengwa na kutaka uchunguzi wa kina kufanya ili kubaini kilichojiri.

Aidha amehoji kuwa ataendelea na jukumu alilotwigwa na bungoma kuangazia usalama wa wakilishi wa bunge la kaunti.

Brian O Ojama

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments