MCA wa chama cha ODM afariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu

Homa Bay
Homa Bay
Mwakilishi wa wadi katika kaunti ya Homa Bay ameaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Chama cha ODM kimethibitisha kifo cha Esther Dwallo ambaye hadi kifo chake amekuwa mwakilishi wadi wa kaunti ya Homa Bay.

Kupitia mtandao wao wa Twitter, ODM ilimsifia sana Esther huku wakisema kwamba alikuwa mwanachama kindakindaki aliyekuwa akijadili masuala muhimu katika bunge la kaunti.

https://twitter.com/TheODMparty/status/1189787702331359232

Esther amekuwa akiugua kwa muda mrefu sana.