Wawakilishi 51 kati ya 107 tayari wamesaini waraka malaum wa kumtimua afisini Elachi nan i sahihi 42 tu zinazohitajika ili kufanikisha hoja ya kumtimua Elachi ambaye wamekuwa wakijaribu kumuondoa madarakani tangu mwaka wa 2018.
Wawakilishi hao wanamshtumu Elachi kwa uongozi unaozua mgawanyiko na kutowaheshemu wanaoshikilia nyadhifa za uongozi katika bunge la kaunti .
“ Elachi anaongoza bunge kw anjia inayozua mgawnayiko ,ufisadi na mwenye makaovu ya kale kulipiza kisasi’ amesema naibu kiranja wa walio wemngi Waithera Chege .
Mwakilishi wa eneo la Utalii Wilson Ochola amemshtumu Elachi kwa kutowaheshimu wawakilishi wa kaunti na kuwakandamiza wale wanapopinga maamuzi yake .
Mwakilishi wa wadi ya Hamza Mark Ndung’u pia amemlaumu Elachi kwa kuleta mgawnayiko kati ya serikali ya kaunti ya Nairobi na Mamlaka ya kusimamia Jiji la Nairobi .
Amesema Elachi ana mazoea ya kuyataja majina ya rais Kenyatta na Raila Odinga ili kuwashurutisha wawakilishi wa kaunti kupitisha maamuzi yake ambayo wengi wanayapinga .