MCA's waTaita Taveta sasa waomba maridhiano na Samboja

NA SOLOMON MUINGI

Baada ya vuta ni kuvute baina ya Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja na wawakilishi wadi hatimaye upande umeona umuhimu wa mashauriano.

Wawakilishi wadi katika kaunti hiyo wamemuomba Samboja kuanzisha mikakati ya maridhiano ili kusuluhisha mzozo ambao unatishia kuvunjiliwa mbali kwa kaunti hiyo. Wakiongozwa na spika Meshack Maghanga, wawakilishi wadi hao walisema kwamba mzozo huo umeathiri pakubwa huduma za kaunti na kusema kuwa vikao vya maridhiano vitasaidia kupatikakana kwa suluhu.

Gavana Granton Samboja alianzisha mchakato wa kukusanya saini kutoka kwa wakaazi wa kaunti hiyo kwa lengo la kuvunjilia mbali serikali ya kaunti hiyo.  Alidai kuhadaiwa na wawakilishi wadi kuhusiana na mipango ya kifedha ya kaunti.

Kwingineko,

Mshukiwa mmoja wa ujambazi anayedaiwa kuwahangaisha na kuwaibia wafanyibiashara mjini Voi, siku ya Jumatatu aliuawa na wananchi waliojawa na ghadgabu, baada ya kufumaniwa akiiba kwenye nyumba moja.

Wananchi walisema kwa muda sasa hali ya usalama umedorora katika eneo hilo na kuitaka idara ya polisi kufanya msako wa mara kwa mara ili kukabili wahalifu wanaohangaisha wafanyibiashara.