McDonald Mariga afunguka kuhusu kustaafu soka. Asema hatumiwi kisiasa

EC6EfXhWwAA5O7w-e1566888673481
EC6EfXhWwAA5O7w-e1566888673481
Staa wa soka na aliyekuwa mchezaji wa timu ya kitaifa Harambee Stars sasa anasema kuwa anaelewa kuntu maisha ya kitongojiduni cha Kibra. McDonald Mariga anamezea mate kiti hiki kilichoachwa wazi baada ya Ken Okoth kuaga.

Iwapo atachaguliwa na Jubilee, staa huyu wa soka atamenyana katika ulingo wa siasa na wawaniaji wa vyama vingine vya ODM, ANC na Ford-Kenya.

Soma hadithi nyingineo:

Siku za kampeni na kujipigia debe tayari zishatajwa. Kuanzia mwezi huu Septemba 9 hadi Novemba 4, wawaniaji hawa watakita kambi mtaa huo wa mabanda kutafuta uungwaji mkono.

"Nimekulia mtaa wa Karanja (eneo linalopatikana katika eneo bunge la Kibra). Naelewa sana hali inavyokuwa kuishi katika mitaa ya mabanda."McDonald Mariga

Soma hadithi nyingineo:

Macdonald Mariga amefika katika ofisi za chama tawala cha Jubilee Pangani leo asubuhi na kuwasilisha stakabadhi zake.

Mariga amekana taarifa kuwa anatumiwa na kiongozi serikalini kugombea kiti hicho.

"Situmiwi na mtu yeyote. Nia kuu ni kuitumikia jamii." Mariga.

Kuhusu kustaafu katika maswala ya soka, staa huyu alikataa kuzungumzia swala hilo.

"Nitawajulisha baadaye kipindi nitakuwa huru kutangaza hilo."