Mcheshi Kelvin Kioko wa Churchill Show asimulia alivyotumia tuzo ya Milioni 1

wwAcN__1575637776_82133
wwAcN__1575637776_82133
Hakika king'aacho kimeundwa! Mcheshi Sammy katika Churchill Show amesimulia kituo hiki jinsi alivyotumia hela aliyoipata katika tuzo za Ultimate Comic.

Sammy ambaye anafahamika kama Kelvin Kioko amesema kuwa lengo kuu lilikuwa kuwaweka sawa wazazi wake ambao walikuwa washatengana kwa sababu ya ulevi wa babake.

https://www.instagram.com/p/B5uTsd9ARMQ/

"Ulevi wa baba ulikuwa serious ikabidi mama akatengana na yeye..." Alisimulia Bustani la Massawe.

https://www.instagram.com/p/B5uv_-_ghHV/

Ushindi wa milioni 1 na gari ulimpa nafasi nzuri ya kuwaweka freshi wazazi wake wawili.

"Babangu alikuwa mlevi kupindukia. Mwanzo ujue akilewa analala kwa ghala. Kwa hivyo nikamjengea nyumba. Mama nikamfungulia duka. Iliyosalia nikalipa karo ya chuo kikuu. Nasomea ualimu..." Amesema Kioko.

Nyota huyu aidha amesema kuwa babake amebadilika na kuacha tabia ya ulevi.

"Siku hizi ako sawa ata alinitumia kunde kutoka nyumbani..." Amesimulia Massawe Jappani.

Mcheshi huyu amepitia hali ngumu ya maisha.

"Nilikuwa nauza viatu Gikomba na pia shuleni ili kupata pesa za matumizi. Ulevi wa babangu ulisababisha matatizo ya kifamilia ukapata karo na chakula ni nadra sana..."