Mchongo wa Mzee Jomo Kenyatta utasalia kwenye noti, sababu zatolewa

unnamed (1)
unnamed (1)

Mahakama kuu imetupilia mbali kesi ya mwanaharakati Okiya Omtatah na mbunge Simon Mbugua ya kubandua picha ya rais wa kwanza Mzee Jomo Kenyatta kwenye noti mpya.

Majaji Kimondo Kanyi na Arsenath Ongeri wamesema kuwa kesi hiyo ilikosa msingi.

Kwa mujibu wa majaji, picha ya Mzee Jomo Kenyatta ipo kwenye picha ya mnara wa KICC (Kenyatta International Convention Centre) ata ingawa ni inatokea kuwa kubwa zaidi.

Soma hadithi nyingine:

Mahakama imesema kuwa mchongo huo sio picha katika noti ila ni sehemu ya KICC.
Majaji wanasema kuwa CBK haijakosea katika kuiweka kwenye noti.

Haya yanahiri huku Benki Kuu ya Kenya ikitilia mkazo kuwa Septemba 30 ndio siku ya mwisho noti mzee za 1,000 zitaacha kutumika.

Wiki mbili zilizopita, Benki Kuu ya Kenya ilitangaza kuwa kuna noti mpya za 1,000 za kutosha .

Soma hadithi nyingine:

Aidha, iliwataka wakenya kuchukua nafasi hii wabadilishe noti hizo katika benki.

Takriban noti Milioni 100 zimerudishwa katika Benki Kuu ya Kenya mwisho wa Agosti.

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Patrick Njoroge aliwaomba wakenya wawakumbushe wakongwe katika jamii wawajibike katika zoezi hilo.