Mdukuzi anayelaumiwa kwa kupoteza bilioni 4 za KRA kujua hatma yake leo

Mshukiwa aliyeshtakiwa kwa kusababisha halmashauri ta ukusanyaji ushuru nchini KRA kupoteza shilingi takriban bilioni nne kwa kudukua mfumo wa KRA Alex Mutungi Mutuku leo atafahamu hatma yake.

Mahakama moja ya hapa nairobi inatarajia kuamua iwapo Mutuku mwenye umri wa miaka 28  ataachiliwa kwa dhamana au kusalia kizimbani kwa siku 40 hadi kesi dhidi yake ianze.

Mutuku  ambaye picha zake mtandaoni zilionyesha maisha ya kifahari amejipata 'maarufu' mitandaoni kwa msemo wake wa 'tumia pesa zikuzoee' lakini udukuzi wake sasa  unatishia kuifikisha safari yake ya mazoea jela.