Mechi saba za kirafiki za kusisimua na kutetemesha ulimwengu

Baada ya msimu kukamilika, timu zote ziliwapa likizo wachezaji wao na sasa likizo zimekamilika huku kukiwa na mechi kadhaa za kirafiki za kukata na shoka msimu huu wa maandalizi ya msimu mpya.

Klabu kubwa Barani ulaya zitakabiliana katika maandalizi yao ya msimu ujao. Mashindano ya international Champions Cup ambayo huandaliwa kule marekani yanatarajiwa kuitetemesha dunia huku pia kukiwa na mechi nyingine za kirafiki.

 1. Chelsea Vs Barcelona tarehe 19

Mechi hii inatagaragazwa nchini Japan tarehe 19 ugani Saitama. Utakua mtihani wa kwanza kwake Frank Lampard kama mkufunzi wa Chelsea kwani mechi alizocheza mbeleni hazina uzito wowote ukilinganisha na mechi za klabu bingwa barani ulaya ama mechi za ligi kuu nchini Uingereza.

Kwa upande mwingine, sajili mpya za Barcelona, Griezmann pamoja na De Jong wanatarajiwa kuonyesha kwa nini walisajiliwa na Barcelona.

 2. Arsenal Vs Real Madrid tarehe  24

Baada ya kusajiliwa na Real Madrid, Eden Hazard atakutana na mtihani wake wa kwanza akivalia jezi ya Real Madrid kwenye mechi dhidi ya Arsenali tarehe 24 kwenye kombe la International Champions Cup.

Hazard anatarajiwa kuwatia motisha mashabiki wa Real Madrid kwenye mechi hizi za kirafiki na inatarajiwa kuwa moja ya mechi hizo ni baina ya Real madrid na Arsenal.

3. Real Madrid vs Bayern Munich tarehe  21

Cristiano Ronaldo aliishi kuwaumiza Wajerumani hawa kila wakati kwenye mechi za klabu bingwa barani ulaya. Hata hivyo, Ronaldo ameigura Madrid na sasa safu ya ushambulizi ya Real Madrid itakua inaongozwa na Eden Hazard  pamoja na Luka Jovic.

Meneja wa Madrid angependa sana kujua iwapo Hazard yupo tayari kuiongoza timu hio kwenye mechi za Laliga na ligi ya Mabingwa Ulaya.

.

4. Arsenal vs Bayern Munich tarehe 18

Kwenye dirisha la usajili, timu hizi mbili hazioneshi juhudi zozote katika kutafta mastaa wa kukiwasha msimu ujao. Hata hivyo, meneja wa klabu ya bayern Munich angependa kuona iwapo timu yake ina uwezo wa kung'anga'nia taji la klabu bingwa msimu ujao.

5. Arsenal vs Barcelona tarehe 4.

Huu ndio utakaokuwa mtihani wa pili kwa vijana wa Barcelona kwenye maadalizi yao ya msimu mpya baada ya kuchuana na Chelsea. Mchuano huu utaandaliwa tarehe nne mwezi Agosti huku mashabiki wa Arsenal wakitarajia kujua iwapo timu yao itawezana kuwania ligi msimu ujao.

6. Liverpool vs Borrusia Dortmund tarehe 20

Wekundu wa Anfield hawana mtihani wowote mgumu kwenye ratiba yao ya maadalizi ya msimu ujao ila Borrusia Dortmund wanatarajiwa kujipima nguvu kujua iwapo wanauwezo wa kulipokonya taji la ligi kuu nchini Ujerumani mikononi mwa Bayern Munich.

7. Juventus vs Atletico Madrid tarehe 10

Baada ya kuwabandua Atletico Madrid kwenye mechi za klabu bingwa barani ulaya msimu uliopita, Juventus itaongozwa na Cristiano Ronaldo kwa mara nyingine kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Atletico madrid  mnamo tarehe kumi mwezi Agosti. Madrid itakuwa inajipima nguvu kujua kama itaweza msimu ujao bila antoinne Griezmann.