Meneja wa Diamond Babu Tale kugombea kiti cha ubunge baada ya kifo cha mkewe

Meneja wa staa wa bongo Diamond Platnumz Babu take anawania kiti cha ubunge, hii ni baada ya WCB kutangaza habari hizo kwenye mitandao yao ya kijamii.

Kupitia kwenye mitandao hiyo lebo hiyo iliposti picha ya Babu na kuandika 'chama cha mapinduzi CCM'.

Hili linajiri siku chache baada ya kumzika mkewe Shamsa.

“CHANGAMOTO NI SEHEMU MOJA KATIKA MAISHA YETU WANADAMU HIVYO KWA CHANGAMOTO NA MITIHANI UNAYOPITIA ISIKUFANYE UKATE TAMAA, ISIKUFANYE URUDI NYUMA SISI TUNAIMANI NA WEWE NA TUNAAMINI UNAWEZA KWASABABU SIFA ZOTE ZA UONGOZI UNAZO.

KWA KIPINDI CHOTE TUMEFAHAMIANA UMEKUWA DEREVA MZURI KWETU NA KWA JAMII PIA NA HILI LIKO WAZI."

Pia lebo hiyo ilisema kuwa atagombea kiti cha ubunge katika mji wa Morogoro.

"NI MUDA SASA WA KUWATUMIKIA WANANCHI WA MKOANI KWAKO MOROGORO VIJIJINI.

USHATIA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MOROGORO VIJIJINI HIVYO CHANGAMOTO NA MITIHANI ULIYONAYO ISIKUFANYE URUDI NYUMA INUKA PANGUSA VUMBI ANZA SAFARI NASI TUKO NYUMA YAKO BEGA KWA BEGA KUHAKIKISHA LENGO LAKO LINAFANIKIWA @BABUTALE MBUNGE MTARAJIWA MOROGORO VIJIJINI #GOTALE #NENDATALE #HAPAKAZITU #TANZANIAYASASA CC @IKULU_MAWASILIANO

@CCMTANZANIA."

Baada ya kuwaongoza wasanii wa lebo hiyo sasa wakati umewadia wa kuwatumikia wananchi.