messi

Messi ajinasua! Mchezaji Messi aihama Barcelona?

Barcelona wamepata pigo kubwa baada ya kiranja wa klabu hiyo Lionel Messi kuripotiwa kufahamisha klabu hiyo kuwa anataka kuondoka msimu huu wa joto.

Messi anaripotiwa kufanya uamuzi wa kuondoka klabu hiyo ambayo imekuwa nyumbani kwa miaka 15 baada ya kufanya mazungumzo na Ronald Koeman.

Inaaminika kuwa bingwa huyo wa Barcelona yuko tayari kumtafuta atakayemsaidia kukatiza kandarasi yake na klabu hiyo.

 

lionel messi

Messi alikumbana na msimu mbaya wakati wa kampeni ya 2019/2020, ambayo ilitokana na kichapo cha aibu kutoka kwa Bayern Munich katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Kwa mashabiki ambao walikuwa wamezoea Messi kuvalia jezi la Barca, watamkosa sana akiondoka kwani ndiye alikuwa fundi wa mabao.

lionelmessi_croppedcuhp0revbful186xobc4hqkumjpg__1561020077_67451

Barcelona wako kwenye mchakato wa kusanifisha klabu hiyo kutoka ngazi za juu huku baadhi ya majina tajika kuwa kwenye hatari ya kuangukiwa na shoka.

“’Sijui kama natakiwa kumshawishi Messi kusalia. Ndiye mchezaji bora duniani na mchezaji ambaye ungependa kuwa naye kwenye timu na huwezi kutaka acheze dhidi yako.” Alizungumza Ronald.

Je Messi anastahili kuhamia klabu ipi kutokana na maoni yako?

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments