Mesut Ozil na Sead Kolasinac wavamiwa na magaidi jijini London

kolasinac
kolasinac
Mshambulizi wa Arsenal Mesut Ozil  na Mlinzi Sead Kolasinac waliponea jaribio la wizi wa Magari hio jana mjini London, Uingereza.

Wawili hawa walikuwa kwenye harakati za kujivinjari baada ya kuwasili jijini London wakitokea Marekani.

Kwenye Kanda ya Video inaonyesha mshambulizi Ozil akijaribu kuhepa na gari huku Kolasinac akiwawekea doria Ozil na ambiria wake ambaye anasemekana kuwa ni bibiye pamoja na mkewe Kolasinac. Magaidi hao walikuwa wamejihamu kwa visu na walikuwa wanasafiri na piki.

Msemaji wa Polisi alieleza vyombo vya habari,

"Hii leo mwendo wa saa kumi na moja jioni polisi waliitwa kuangalia tukio ambapo majambazi waliojihamu na visu walijaribu kuwavamia wanaume wawili na familia zao. Hata hivyo wawili hao waliponea tukio huilo bila majeraha."

Klabu ya Arsenali pia ilidhibitisha jambo hilo na kusema kuwa wachezaji hao hawakuadhirika hivo walitarajiwa mazoezini kama kawaida.