Mfanyakazi wa machimbo Naivasha apigwa katika vipande na mlipuko

Mfanyakazi wa machimbo alipigwa katika vipande Naivasha baada ya mlipuko kulipuka ulipokuwa ukianzishwa.

Hisia za familia na wenzake waliokuwa wakifanya kazi na yeye zilikimbia juu, kabla ya polisi kuenda kuchukua mabaki ya mwili na kupeleka katika chumba cha kuifadhi maiti cha Naivasha.

Tukio hilo linakuja tu baada ya mwanaume kuangamizwa na mwamba kisha akakufa katika machimbo ya karibu na Naivasha maeneo ya Maraigushu.

Katika tukio hilo la awali mwanaume huyo aliweza kufariki baada ya ajali ya mlipuko huo ulipokuwa ukianzishwa pia wenzake kukimbilia usalama wao.

Kulingana na Jackson Mathenge, ilikuwa kawaida kwa wanyakazi hao kutumia mlipuko ili kuvunja miamba hiyo ambayo hutumiwa baadaye kama mawe ya kujengea.

Alisema pia hawajabaini wazi nini kilicho sababisha mlipuko huo kwa maana imekuwa sasa kwa muda kama kitendo hicho hakijatendeka.

"Kulikuwa na mlipuko mkubwa na marehemu kukatwa kwa vipande na kufa papo kwa hapo kutokana na athari za kulipuka," Alisema Mathenge.

Wakati huohuo wakazi wa eneo la Longonot, Naivasha wanaitaka serikali ya kaunti kuimarisha usalama wa eneo hilo baada ya mauaji ya mwanaume wa miaka, 82, na mwana bodaboda.

Akiongea wakati wa mazishi ya mwanaume anaye fahamika kama Absolom Mburu, viongozi wa eneo hilo waliweza kuwashutumu  wafugaji majirani wa kaunti ambazo zimo karibu na wao.

Mwendesha pikipiki huyo aliweza kuuwawa wiki mbili zilizopita na pikipiki yake kuibiwa, kabla ya mkulima huyo kuuwawa na migugo yake pia kuibiwa.

Akiongea katika mazishi mchungaji Peter Thuku alibaini kuwa katika visa hivyo viwili vimetendeka na hakuna mshukiwa hata yeyote ambaye ameweza kukamatwa au kutiwa baroni, jambo ambalo limefanya wakazi wawe na wasiwasi wa maisha.

Alisema kuwa wiki kadhaa ambazo zimepita wafugaji waliweza kuja katika maeneo hayo wakiuliza kulisha mifugo yao eneo hilo, kisha kuleta vurugu kati ya wafugaji na wakulima wa eneo hilo.

"Katika kesi zote mbili tunaamini baadhi ya wafugaji wameweza kutekeleza kitendo na tunawauliza polisi waweze kuingilia kati kabla ya wanakijiji kupoteza maisha zaidi," Alisema  Peter.