Mfanyibiashara mashuhuri Nairobi, ajipata mashakani kwa kumtumia mpenzi wa zamanani picha zake akiwa uchi

Je unaweza kumtumia aliyekuwa mpenzi wako picha zako ukiwa uchi wa mnyama?

Ukistaajabu na hayo basi jamaa mmoja ambaye ni mfanyibiashara mashuhuri mjini Nairobi amejipata mshakani baada ya kujaribu kumvutia tena aliyekuwa barafu yake ya roho kwa kumtumia picha zake akiwa uchi kupitia barua pepe.

Soma habari zaidi;

Mwanamume huyo ambaye jina lake tumelibana alifikishwa katika mahakama ya Kibera akishtakiwa kwamba mnamo Julai 5 mwaka huu alimtumia aliyekuwa mpenzi wake picha zake akiwa amevalia suti yake ya kuzaliwa hatua ambayo kulingana na upande wa mshataka ilimkera mno mlalamishi.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 58 anakabiliwa na mashtaka chini ya sheria ya uhalifu wa mtandao kwa unyanyasaji.

Soma habari zaidi;

Pia anashtumiwa kwa kuzituma picha hizo chafu kwa marafiki wa aliyekuwa mpenzi wake, baadhi ya marafiki walipata picha hizo kupitia WhatsApp na tayari wameandikisha taarifa.

Mshukiwa hata hivyo alikanusha mashtaka mbele ya hakimu mkuu wa Mahakama ya Kibera Abdul Lorot na kudai kwamba wanasuluhisha jambo hilo nje ya mahakama. Kesi inaendelea.