Mfuateni mgombeaji wenu Orange House,Ruto awaambia wakosoaji

ruto
ruto
Naibu wa  Rais  William Ruto  siku  ya  jumamosi amewakemea wanachama wa Jubilee wanaomuunga mkono  Raila Odinga kugombea tena urais  akisema kwamba wanafaa kujiuzulu kutoka chama hicho .

Akizingumza na wahubiri wa kiislamu katika hoteli ya Pride inn huko Shanzu Mombasa   Ruto amesema wanachama wa Jubilee wanaompigia debe mgombeaji mwingine  wanakiuka  msimamo wa  chama  hicho .

" Iwapo  mgombeaji wako yuko  Orange House  mnafanya nini Jubilee? Nendeni Orange House!’ Alisema Ruto

Alikuwa akiwajibu wale waliomtaka ajiuzulu kama naibu kinara wa chama  na Naibu wa Rais

Naibu mwenyekiti  David  Murathe  na mbunge wa  Nyeri mjini Ngunjiri Wambugu  ni miongoni mwa viongozi waliomtaka Ruto kujizulu  wakisema anakiuka  kila msimamo wa mkuu wake Rais Uhuru Kenyatta .

Ruto  aliwataka  wafuasi wake  wanaoteswa kwa sababu ya kumuunga mkono  kusalia  na ukakamavu .

Alisema  chama cha Jubilee kina wanachama milioni nane  na kinawahudumia wakenya milioni 45 hivyo basi hakuna anayefaa kumtisha  yeyote .