Mgala Muuwe Na Haki Umpe: Wanabodaboda Kunyanyaswa Mutungu Kaunti Ya Kakamega

Kila uchao binadamu hujihusisha na shughuli za hapa na pale ili kujikimu  kimaisha kwa kutafuta riziki. Waswahili walisema kazi ni kazi, isitoshe kulingana na uchumi unvyozorota lazima utie bidii kwa kila jambo unalolifanya kwani mtegemea cha nduguye hufa maskini.

Wahudumu wa bodaboda kutoka eneo la Matungu kaunti ya Kakamega na Butula hii leo wameandamana hadi makao ya naibu kamishna wa gatuzi ndogo la Butula kulalamiia kunyanyaswa na maafisa wa utawala wa Butula barabarani.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao James Musebe na kiongozi wa vijana wa Matungu Wycliffe Wafula, wanabodaboda hao zaidi ya mia mbili wanadai kuwa maafisa hao huwatosa kati ya shilingi hamsini na mia tano katika kizuizi cha barabara karibu na soko la Ogalo.

Wahudumu hao wanadai kuwa wameshindwa kujimudu kimaisha kutokana na kunyanyaswa na polisi na kutaka malalamishi yao yashughulikiwe.

Msaidizi wa naibu kamishna wa Butula Jackson Oloo aliandaa kikao na viongozi wa wahudumu hao na kupokea malalamishi yao kabla ya kuwahutubia wahudumu hao na kuahidi kutoa suluhu baada ya siku tatu zijazo.

Maafisa wa polisi wahehusishwa na visa vingi sana za kupokea hongo kutoka kwa wanainchi, hali hii imesababisha kuongezeka kwa ufisadi na utovu wa nidhamu katika sekta ya usafiri. Tafakari kwa nini ajali nyingi imekithiri kwa kimo cha juu katika barabara zetu?