Mhadhiri Apatikana Akiwa Amefariki Nyumbani Kwake Baada Ya Siku Tano

Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi baada ya mhadhiri wa taasisi ya teknolojia ya Siaya kupatikana nyumbani kwake siku tano baada ya kufariki.

Mwili wa mhadhiri huyo kwa jina James Nyarage mwenye umri wa miaka 55 ambaye alikuwa akiishi pekee yake uligunduliwa na jirani baada ya siku tano.

Kulingana na jirani yake,  marehemu alitoweka kwa siku tano kabla ya kuanza kusikia uvundo ukitoka nyumbani kwake na kuamua kuvunja mlango wake.

Akithibitisha kisa hicho OCPD wa Siaya Ancent Kaloki alieleze kuwa huenda marehemu alifariki siku tano zilizopita nyumbani kwake bila majirani kufahamu.

Aliongezea kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo kamili cha kifo chake.

-Lameck Baro