MIA: ‘Alinitoroka siku ya harusi, sasa anataka turudiane, never!” Mwanamke amkemea jamaa aliyehepa siku ya harusi

pulpit
pulpit
Faith Bosibori  hajapunguza hamaki  yake dhidi ya aliyekuwa mchumbake Alex  Matano ambaye alimfanyia kitendo kibaya kwa mwanamke yeyote alimuacha kwenye pulpit na kukwepa siku yao ya harusi .

Sasa Alex amewaza na anajutia alichofanya Agosti tarehe 23 mwaka wa 2017 na anataka kurudiana naye ili tena waendelee na uchumba wao na baadaye wakamilishe walichokuwa wameanza kanisani. Kwanza, Faith anasimulia kilichojiri na mbona hataki kumuona hata machoni Alex kwa kitendo hicho ambacho kwake alikichukulia kama madharau na jambo ambalo lilimfedhehesha mbele ya jamaa zake, wenzake  wa kazini na wanakijiji kizima huko Ogembo .

Harusi yao kama harusi nyingine, ilikuwa imepangwa kwa muda mrefu na hafla nyingi za kuchangisha fedha. Kitu ambacho kilimfanya Alex Kgeuza mawazo  dakika za mwisho mwisho ni kwamba Faith alikuwa anakimbilia sana harusi hasa baada ya kugundua kwamba alikuwa mjamzito. Alex alikuwa akitaka kwanza  wapate mtoto huyo kisha baadaye wapange harusi lakini mchumbake hakusikia hilo na hapo ndipo ngoma ilipoanza na sakata ikazuka. Faith na jamaa zake walichukua usimamizi wa shughuli zote za kuandaa harusi. Pingamizi  na ushauri wa  jamaa za Alex  zilipuuzwa na hapo ndipo watu wa Alex walipoamua kupanga njama ya kuhakikisha kwamba harusi hiyo inatibuka ili iwe adhabu kwa Faith na jamaa zake waliokuwa wanataka msichana wao aolewe kabla ya mwanao Alex kuwa tayari .

Ingawa Alex anajutia kilichofanyika, anasema wakati huo mpenzi wake alifanya makosa kwa kukata kumsikiliza au hata kufuata ushauri wake wa kuahirisha harusi. Faith anasema hakutaka kumzaa mtoto wake nje ya ndoa kwa sababu ya  shinikizo ya kifamilia kwani babake alikuwa askofu wa kanisa moja linaloheshimika

‘Ingekuwa aibu kwa wazazi wangu na familia iwapo mimi mtoto wa askofu ningezaa kabla ya kuolewa’ anasema Faith

Wakati ilipogundulika kwamba itakuwa vigumu kumzuia Faith kukubali harusi iahirishwe, Alex na jamaa zake walikula njama ya kuhakikisha kwamba siku ya harusi haonekani na hivyo ndivyo ilivyofanyika .

Saa saba kamili Alex alifaa kuwa amefikishwa kanisani na wapambe wa bwana harusi lakini wakati huo, alikuwa amepanda basi kwenda Isebania kwa  mjombake ili kutuliza fikra na kumkwepa Faith ambaye tayari alikuwa kanisani. Watu wa Faith walikuwa tayari wamejaa kanisani na katika ukumbi ambao sasa maankuli yangeandaliwa . Hata hivyo, waligundua kwamba kuna tatizo wakati walipogundua kwamba rafiki zake Alex  na baadhi ya jamaa zake hawakuwa kanisani wakati ule. Kabla hawajaanza kuunganisha moja na mbili ili kupata tatu, padre wa kusimamia harusi yao aliingia na pale ikagundulika kwamba bwana harusi hayupo  na simu yake ni mteja .

Faith aliishiwa nguvu  akiwa pale katika jukwaa la kanisa ambako alitarajia kula kiapo cha ndoa na mumewe na sekunde chache baadaye alijikuta chini ya mti nje ya jengo la kanisa akipepetwa. Alikuwa kazimiwa na sasa fahamu zake zilipomrudia aliunganisha kwa sekunde moja kwamba Alex amemkwepa na kumuacha kwenye pulpit siku ya harusi yao. Papo hapo, Faith alikata kauli kutomuamini mwanamme yeyote na imekuwa  vita vya nafsi na moyo wake kuanzia wakati masaibu hayo yalipomkuta. Ili kufungua jeraha  ambalo halijapona, Alex amerudi sasa na anataka msamaha..Niokotwe!