MICHEZO: Man U yamsajili Ighalo, Shujaa yaanza vibaya mashindano ya Sydney 7s

ighalo
ighalo
Timu ya raga ya Kenya sevens ilianza kampeni yao ya msururu wa IRB Sevens mkondo wa Sydney kwa kunyukwa alama 28-14  na Fiji asubuhi ya leo huku New Zealand wakichukua uongozi wa kundi lao kwa ushindi wa 54-5 dhidi ya Wales.

Mechi ya pili ya Shujaa itakua dhidi ya Wales saa 12.05, kabla ya kumaliza udhia kesho saa 5.41 jioni dhidi ya mabingwa wa Hamilton 7s New Zealand.

Msururu wa habari za michezo

Mshambulizi wa AFC Leopards John Makwata amejiunga na miamba wa ligi ya Zambia Super League, Zesco United. Makwata ambaye ndio mfungaji bora wa mabao kwenye klabu hio ametia saini mkataba wa miaka mitatu na timu hio ya Ndola.

Anaungana na wakenya wenzake kipa Ian Otieno aliyejiunga nao msimu huu kutoka Red Arrows, Jesse Were na David Owino ambao wamekuwa katika klabu hio kwa zaidi ya misimu minne sasa.

Dirisha la uhamisho la Uingereza la mwezi January limefungwa saa nane alfajiri ya leo huku hakuwa. Manchester United walifikia mkataba na raia wa Nigeria Odeon Ighalo wa mkopo wa miezi sita kutoka timu ya Uchina Shanghai Shenhua, huku Nathan Bishop akisajiliwa kutoka Northend.

Danny Rose amehamia Newcastle kutoka Tottenham huku Chelsea wakishindwa kumpata mshambulizi Edison Carvani ambaye anasalia na mabingwa wa Ufaransa PSG.

Kwingineko huko Uropa Yanack Carrasco amehamia Atletico Madrid kutoka Uchina, huku Emre Can akihamia Borussia Dortmund kutoka Juventus wote wawili kwa mkopo.

Malkia strikers watalazimika kujibidiisha ili kufuzu kwa nusu fainali ya michuano ya Olimpiki ya mwaka huu, baada ya kuwekwa kwenye kundi moja na wenyeji Japan, Brazil, mabingwa wa Uropa Serbia, Korea na Jamuhuri ya Dominican katika kundi A.

Malkia strikers ambao wanaregea kwa michezo hiyo ya msimu wa joto baada ya miaka 16 walishinda michuano ya kufuzu mwezi uliopita jijini Yaunde na kujikatia tikiti ya pekee barani Afrika. Mabingwa wa dunia Uchina watapambana na Marekani, Urusi, Italia, Argentina na Uturuki katika kundi B.