Michezo. Pep aomboleza kifo cha mamake kilichosababishwa na Corona

NA NICKSON TOSI

Kocha mkuu wa Klabu ya Manchester City Pep Gaurdiola anaomboleza kifo cha mamake mzazi Dolors Sala aliyefariki baada ya kukabiliana na virusi vya Corona kwa muda.

Dolors Sala anaaminika kufariki dunia kutokana na virusi vya corona akiwa na miaka 82.

Kifo chake kinajiri wiki moja tu baada ya Pep kutoa kima cha lake pauni 920,000 kama mchango kwa serikali ili kufanikisha vita dhidi ya virusi hivyo.

Klabu ya Manchester City ilitangaza habari hizo za kusikitisha siku ya Jumatatu, Aprili 6, kabla ya kutuma risala za rambirambi kwa meneja huyo Muhispania.

Kwa sasa, ligi kuu ya Uingereza imesitishwa kutokana na virusi hivyo ambavyo vimeathiri idadi kubwa ya wananchi wa taifa hilo .

Yanajiri haya huku vilabu vinavyoshiriki katika ligi kuu ya Bundesliga vikirekijea mazoezi yao baada ya kusimamishwa kwa muda.