Francis Kimanzi akabidhiwa mikoba ya Harambee stars kwa miaka miwili

Francis.Kimanzi.Zedekiah.Otieno
Francis.Kimanzi.Zedekiah.Otieno
Shirikisho la soka nchini FKF limekabidhi Francis Kimanzi tena mikoba  ya kuiongoza timu ya taifa, Harambee stars kwa muda wa miaka miwili. Kimanzi alikuwa kocha wa stars mwaka wa 2011 hajafururshwa kufuatia msururu wa matokeoa duni.

Francis Kimanzi amekuwa kocha wa nne sasa tangu Nick Mwendwa kupewa majukumu ya kuiongoza shirikisho hilo. Awali,Kenya ilikuwa imewaajiri Paul Put, Stanley Okumbi pamoja na Sebastiane Migne. Jukumu lake Kimanzi litakuwa ni kuirejesha timu ya stars kwenye mashindano ya AFCON 2021.

Kocha wa Sony Sugar, Zedekiah Otieno atakuwa kocha msaidizi wake Kimanzi huku Lawrence Webo akiwa kocha wa walindalango. Enos Karani pia atajiunga na benchi la kiufundi la stars kama kocha wa kuangazia hali ya afya ya wachezaji.

Mechi ya Kwanza ya kimanzi itakuwa dhidi ya Uganda mnamo tarehe nane mwezi septemba ugani Kasarani hapa mjini Nairobi huku hio ikifuatiwa na mechi dhi ya Libya pamoja na mechi za kufuzu kwa michuano ya AFCON 2021 dhidi ya Togo na Egypt.