Tetesi za mastaa barani Ulaya 23/08/2019

Dirisha la uhamisho linalelekea kukamilika tarehe 1 mwezi septemba. Kumekuwa na biashara za kiusajili za mastaa kadha barani ulaya.

Victor Wanyama

Kiungo huyu mkabaji anasemakana kuwa tayari kujiunga na klabu ya Club Brugge ya Ubelgiji kwa ajili ya kujitafutia muda wa kucheza. Totenham ilimsajili kiungo wa Ufaransa, Tanguy Ndombele hivyo kuyafanya maisha yake Wanyama kuwa magumu ugani White hart lane kwa kufinya nafasi  za kucheza. Wanyama huenda atalazimika kukubali kukatwa mshahara ili kuweza kufanikisha uhamisho huo.

 Neymar

Klabu ya PSG imekataa ombi la Real Madrid la kumsajili Neymar kwa ada ya pauni themanini na nane pamoja na mcheza james Rodriguez. PSG imesema kuwa fedha hizo ni ndogo sana huku wakidai kuongezewa mshambuli Gareth Bale ili kuweza kukubali ombi hilo.

Hirvin Lozano

 Klabu ya Napoli inaelekea kukamilisha usajili wa mshambulizi a timu ya taifa ya Mexico na Psv, Hirvin Lozano mwenye umri wa mika 22. Lozano aliisaidia klabu yake kumaliza katika nafasi ya pili kwenye ligi kuu nchini Uholanzi msimu uliopita huku akitajwa kama talanta mpya jikoni.

Islam Slimani

Aliyekuwa mshambulizi wa Leicester City, Islam Slimani amekamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya AS Monaco kwa mkopo wa mwaka mmoja. Slimani mwenye umri wa miaka 31 alisaidia taifa lake kushinda kombe la AFCON. Slimani amekuwa mchezajiwa tatu kusajiliwa na klabu ya Monaco  msimu huu baada ya Wissam Ben Yedder na Henry onyekuru kutoka Chelsea.

 Alexis Sanchez

Mshambulizi wa Manchester United, Alexis Sanchez huenda akajiunga na klabu ya Inter Milan kulingana na gazeti la Manchester Evening. Sanchez amekubwa na utata mwingi tangu ajiunge na miamba hio ya soka ya uingereza.

Mustafi

Mkufunzi wa Arsena, Unai Emery amewaambia wachezaji, Schkodran Mustafi pamoja na Mohammed Elneny wameruhusiwa kutafuta klabu nyingine. Hali ya Elneny na Mustafi imekuwa ya ati ati huku mkufunzi wao akijitokeza hadharani kudai kuwa asha waeleza hali ilivyo. (Skysports).