Guardiola angeshinda mataji yote kama angeteuliwa kocha wa Uingereza - Rooney

rooney
rooney
Mshambuliaji wa zamani wa England Wayne Rooney anaamini Pep Guardiola angeshinda vikombe vyote iwapo angepewa ukufunzi wa timu ya Uingereza. (Manchester Evening News)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane atanataka kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante, 28. (The Athletic, subscription required)

Manchester United wanamchunguza kiungo wa kati wa Leicester City James Maddison kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 msimu ujao. (Manchester Evening News)

Liverpool, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich zinamnyatia kiungo wa kati wa Napoli Fabian Ruiz, 23. (Calciomercato, via Daily Mail)

Nahodha wa zamani wa klabu ya Chelsea John Terry amepigiwa upatu na mkufunzi wa zamani Roberto Di Matteo kuwa mkufunzi wa klabu hiyo katika siku za usoni. (Athletic, via Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Chelsea Willian anaamini timu yake ina uwezo wa kushinda taji msimu huu licha ya mkufunzi mpya Frank Lampard kushika hatamu katika hali ngumu. (Standard)

Manchester United imeandaa kuongeza maradufu mshahara wa Victor Lindelof, 25, na kumpatia kandarasi ya mshahara wa £150,000 kwa wiki. (Sun)

Mkufunzi wa England Gareth Southgate anasema kwamba mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy huenda akarudi katika kikosi cha taifa licha ya kutangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa mwaka uliopita . (Times, subscription required)

Beki wa zamani wa Arsenal Per Mertesacker ametoa wito kwa kiungo wa kati Asrenal Mesut Ozil, 30, kuimarika na kutoa mchango wake kwa klabu hiyo , akisema kwamba ana kipaji ambacho hakina mchezaji mwengine wa Arsenal. (Talksport)

-BBC