Yaani hata Kamami! Tazama picha za mpango wa kando wa Terence Creative

Kupitia mitandao ya kijamii ni wazi kuwa mcheshi Terence Creative ajulikanaye sana kama Kamami ana mpango wa kando na ata amekubali madai ya kuenda nje ya ndoa.

Milly Chebby na mpenzi wake Kamami wamekuwa na misukosuko katika ndoa yao kwa sababu ya kidosho Anita ambaye ndiye mpango wa kando wa bwana Terence.

Baada ya aibu ya Terence kupatikana na mpango wa kando, bwana huyu kupitia mtandao wa kijamii amefungukua wazi na kusema wazi anavyo mpenda mke wake.

Binti ambaye ametia bwana Kamami kwenye aibu chungu nzima ni binti mwenye umri wa miaka 19.

Amini usiamini, mpango wa kando wa bwana Terence ana umri wa miak 19 na wakishirikiana, hawakuwa wanaona kama ni tatizo kwani wahenga walisema, mapenzi ni kipofu!

Zaidi ya hayo, hata ikiwa binti huyu amejitia aibu na kumfanya Terence aingie matatani, siwezi kumlaumu bwana Kamami kwani binti huyu Anita ni mrembo sana, yaaani katoto hodari .

Hebu tazama picha