Anaenda Arsenal? Jose Mourinho yuko tayari kurudi ligi ya Uingereza

Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho yuko tayari kurudi katika soka ya Uingereza kutokana na lengo lake la kutaka kushinda mataji katika ligi ya Premia.

Mourinho pia ana hamu ya kuchukua uongozi wa klabu ya Arsenal iwapo ipo.

FIFA imewakumbusha marefa kutumia marejeo ya msaidizi wa Video, VAR kabla ya kubadilisha maamuzi muhimu. VAR hutumiwa katika angalau nchi 25, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la FIFA na Ligi ya Mabingwa ya UEFA.

Baraza linaloongoza mpira duniani limethibitisha kuwa bado linapendekeza utumiaji wa video hizo kabla maamuzi hayajabadilishwa na marefa. Kwenye Ligi Kuu, maamuzi 26 yalipinduliwa katika michezo 100 ya kwanza kutumia VAR msimu huu.

Suala hilo litajadiliwa katika mkutano wa vilabu vya Ligi Kuu Novemba tarehe14.

Kipa wa Southampton na England Fraser Forster, mwenye umri wa miaka 31, yuko tayari mshahara wake kupunguzwa ili kuendelea na kazi yake katika klabu ya Celtic kwa kandarasi ya kudumu.

Leicester na Watford ni miongoni mwa klabu zinazomnyatia Ronald Sobowale - mpwa wa mchezaji wa Bayern Munich na nyota wa Austria David Alaba. Sobowale, 22, anaichezea timu ya daraja la nane katika ligi ya Bostick klabu ya kusini mashariki na pia amefanyiwa majaribio na klabu ya Middlesbrough.

AC Milan iko tayari kuwasilisha ombi lingine la kujaribu kumsaini beki wa Liverpool na Croatia Dejan Lovren, 30.

Leicester na Watford ni miongoni mwa klabu zinazomnyatia Ronald Sobowale - mpwa wa mchezaji wa Bayern Munich na nyota wa Austria David Alaba. Sobowale, 22, anaichezea timu ya daraja la nane katika ligi ya Bostick klabu ya kusini mashariki na pia amefanyiwa majaribio na klabu ya Middlesbrough.

Klabu ya Ujerumani ya Schalke inataka kumzuia kuondoka mchezaji wa klabu ya Everton ambaye yupo kwa mkopo katika klabu hiyo Jonjoe Kenny kusalia zaidi ya msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yupo kwa mkopo wa kudumu.