Bayern Munich wamwachisha kazi meneja Niko Kovac baada ya kunyukwa 5-1

Bayern Munich wamemwachisha kazi meneja Niko Kovac. Uamuzi huo unafuatia kunyukwa kwao mabao 5-1 na Eintracht Frankfurt, jumamosi. Kovac anaiwacha Bayern ikiwa katika nafasi ya nne kwenye jedwali, alama nne nyuma ya viongozi Borussia Monchengladbach.

Meneja huyo alikua kwenye usukani kuanzia Julai mwaka 2018.

Kiungo wa kati ya Everton Andre Gomes alipata jeraha baya la mguu lililomwacha Son Heung-min wa Tottenham na machozi na kuweka dosari bao lao (Everton) la kusawazisha na kujipatia alama muhimu.

Gomes aligongwa na Son na akaonekana kuumia baada ya kuanguka vibaya hali iliyosababisha malalamishi kutoka kwa wachezaji na mashabiki waliokua karibu. Son aliondolewa na refa huku Gomes akipata matibabu na kisha kuondolewa kwa machela.

Bandari walibanduliwa nje ya kombe la Caf Confederation baada ya kunyukwa 1-0 na Horoya jijini Nairobi jana. Ocansey Mandela alifunga bao hilo la Guinea na kuwasaidia kufuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-2 baada ya kufunga 4-2 katika mkondo wa kwanza. Fred Nkata alifanya mashambulizi muhimu kunako dakika ya 13 baada ya Horoya kupata bao lao.

Gor Mahia wamebanduliwa nje ya kombe la Caf Confederation baada ya kufungwa 2-1 ugenini na DC Motema Pembe katika mkondo wa pili wa mechi ya kufuzu.

Mabingwa hao wa KPL walikua wanahitaji ushindi au sare ya mabao mengi ili kufuzu kwa awamu ya makundi, baada ya kutoa sare ya 1-1 katika mkondo wa kwanza jijini Nairobi. DR Congo walihitaji sare tasa au ushindi wa aina yoyote ili kufuzu.

Meneja wa Chelsea Frank Lampard ameonya kuwa utumizi wa sasa wa VAR unaweza kuwa hatari kwa ligi ya Primia. Mwongozo kutoka kwa ligi ya Premier mwanzoni mwa msimu ilisema kuwa VAR itatumika tu kwa makosa ya wazi ya marefa wa uwanjani. Lakini wakati Watford walipewa penalti na VAR baada ya Gerard Deulofeu alipotegwa na Jorginho, Lampard anasema alishangazwa sana.

Watford huenda wanahisi kuwa walifaa kupewa uamuzi huo baada ya kunyimwa penati, aliyopitiwa na VAR katika mechi yao waliyotoka sare ya 1-1 dhidi ya Tottenham mwezi uliopita.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola anasema wachezaji wa Liverpool watakua wanajitosa kushinda mechi, siku kadhaa kabla ya timu hizo mbili kukutana ugani Anfield. Viongozi wa ligi ya Premier  Liverpool watawaalika mabingwa City tarehe 10 mwezi huu. Sadio Mane alifunga bao kunako dakika ya 94 na kuwapa the Reds ushindi dhidi ya  jumamosi.