Rekodi ya asilimia 100 ya Arsenal yafika kikomo katika ligi ya Europa

Arsenal
Arsenal
Rekodi ya asilimia 100 ya Arsenal katika ligi ya Uropa msimu huu ilifikia kikomo wakati Bruno Duarte alipofunga bao kukano dakika ya 91 na kusawazishia Vitoria Guimaraes huko Ureno.

Shkodran Mustafi alikua amefungia the Gunners bao huku ikiwa imesalia dakika 10 mechi hio kutamatika. Lakini  Guimaraes wakajikakamua na kufunga bao. Arsenal bado watafuzu kwa 32 bora leo iwapo Standard Liege watapoteza kwa Eintracht Frankfurt.

Kiungo wa Brazilian Rodrygo alitamba kwa kufunga mabao matatu, Real Madrid walipowaadhibu Galatasaray mabao 6-0 katika ligi ya mabingwa. Kinda huyo wa miaka 18 amekua mchezaji mchanga zaidi kufunga mabao matatu katika ligi hiyo.

Karim Benzema alifunga mabao mawili. Kwingineko Juventus walifuzu kwa 16 bora kawenye ligi hio kwa kuwanyuka Lokomotiv Moscow 2-1 katika kundi D.

Manchester City walitoka sare ya 1-1 Atlanta huku Paris St. Germaine wakiwanyuka Club Bruges 1-0.

Huenda Serie A ikakubali wachezaji watano kubadilishwa katika mechi, baada ya ombi kuwasilishwa na shirikisho la soka la Italia. Hatua hio inaungwa mkono na vilabu vikubwa vya Italia ambao wanataka kuwa na chaguo zaidi huku timu tayari zikiruhusiwa kuwataja wachezaji 12 kwa benchi. Mabadiliko hayo matano yatafanyika mara tatu ili kupunguza idadi ya muda wa mapumziko katika mechi.

Mathare United waliwapa Gor Mahia kichapo chao cha kwanza msimu huu katika ligi ya KPL, kufuatia ushindi wao wa 1-0 jana mchana ugani Machakos. Gor walianza mechi vizuri lakini Mathare wakachukua fursa za mapema na kufunga bao. Kwingineko Western Stima waliwashangaza Bandari kwa kuwanyuka mabao 3-1 katika mechi iliyochezwa Kisumu.

Kambi ya Harambee Stars imepigwa jeki na kuwasili kwa wachezaji wawili wanaosakata soka Uswidi Eric Ouma na Joseph Okumu. Ouma anasema wamewasili mapema kwa kua ligi yao tayari imekamilika na tayari wameshafanya mazoezi na kikosi hicho. Ouma falichezea Vasalund wikendi iliyopita walipopata ushindi wa 3-1 dhidi ya Sandkiven huku Okumu akiwa hakucheza katika mechi ya IF Elfsborg waliyoshinda Helsingborg.

Wapinzani wa Harambee Starlets katika raundi ya nne ya michuano ya kufuzu kwa Olimpiki, Shepolopolo ya Zambia waliwasili nchini jana. Pande hizo mbili zitakabana kesho uwanjani Kasarani katikia mkondo wa kwanza wa michuano hio. Wazambia watakua wenyeji wa mkondo wa pili siku nne baadae uwanjani Nkoloma jijini Lusaka. Mshindi wa jumla atafuzu kwa raundi ya mwisho ambapo atakutana na aidha Cameroon au Ivory Coast. Mshindi wa raundi ya mwisho atafuzu kwa michuano ya olimpiki jijini Tokyo mwaka 2020.