Guardiola athibitisha kuwa atakosa huduma za mshambulizi Sergio Aguero

aguero
aguero
Meneja wa Machester City Pep Guardiola amethibitisha kuwa mshambulizi Sergio Aguero hatakuwepo kwa timu wiki zijazo baada ya kupata jeraha pajani katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Chelsea Jumamosi iliyopita.

Pep ameongeza kuwa itakua muujiza iwapo  Aguero ataweza kurejea michezoni akiwa katika hali thabiti katika mechi yao dhidi ya Manchester United tarehe 7 mwezi  ujao.

Mshambulizi Gabriel Jesus anatarajiwa kuchukua nafasi ya Aguero wakati huu na pia kuongoza watakapochuana na Shakhtar kwenye ligi ya mabingwa wiki hii.

Jose Mourinho ametupilia mbali tetesi za Zlatan Ibrahimovic kujiunga na klabu ya Tottenham.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 aliisaidia Manchester United kushinda kombe la ligi kuu barani Uropa chini ya usimamizi wa Mourinhno. Kadhalika Spurs itachuana na Olympiakos katika ngome yao hii leo juma moja tu baada ya klabu hiyo kumpiga kalamu Mauricio Pochettino.

Tottenham inamfuatilia mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake mwenye umri wa miaka  24, huku beki huyo Mdachi akipigiwa upatu kuchukua nafasi ya Jan Vertonghen, ambaye kandarasi yake ya Spurs inakamilika msimu wa joto wa mwaka 2020.

Kwingineko, Arsenal huenda ikamkosa beki wa kati wa Barcelona Samuel Umtiti, mwenye umri wa miaka 26, huku kiungo huyo wa Ufaransa akinuia kurejea katika klabu yake ya zamani ya Lyon ikiwa ataamua kuondoka Nou Camp.

Shirikisho la kandanda nchini, FKF litawaandalia wachezaji wa timu ya kitaifa ya kinadada Harambee Starlets chakula cha mchana katika hotel ya Utalii kufuatia ushindi wao baada ya kuitinga Tanzania mabao mawili kwa nunge wakiwa kwao kwenye finali za CECAFA.