Ligi ya mabingwa Ulaya: Lampard atawafikisha Chelsea katika mkondo utakaofuata?

Raundi ya sita ya ligi ya mabingwa Ulaya itakuwa inachezwa leo usiku huku wakufunzi kutoka klabu mbalimbali wakiwa na shinikizo ya kufika katika ngazi utakaofuata baada ya michuano ya vikundi.

Vijana wake Frank Lampard watakuwa wanawakaribisha klabu ya Lille nyumbani kwao ugani Stamford Bridge.

Chelsea ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu katika kundi H wakiwa na pointi 8, watakuwa na kibarua kigumu leo usiku kwani wanastahili kushinda mechi hiyo ndiyo wafaulu kufika katika mkondo utakaofuata.

 Lille kwa upande wao wanashikilia nafasi ya 4 wakiwa wameandikisha pointi 1 pekee.

Lampard ataweza kuutegua kitendawili hicho?

Mechi zingine zitakazochezwa leo usiku ni;

Red Bull vs Liverpool

Dortmund vs Slavia Praha

Ajax vs Valencia

Intermilan vs Barcelona